Uongozi wa Simba umeeleza kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa mtendaji wake mkuu, Dk Anorld Kashembe.
Taarifa iliyotolewa na Simba leo Jumatatu Desemba 23, 2024 imeeleza kuwa wamepoteza mtu ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa klabu hiyo.
“Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya msiba uliotokea leo 23.12.2024 wa aliyekuwa Mtendaji wa klabu Dk Anorld Kashembe.” Imeandika taaria hiyo.
Aidha, Dk Kashembe alikuwa CEO wa Simba kuanzia 2019 hadi 2021 ambapo aliiongoza kwa mafanikio makubwa.
Chini ya utumishi wa Dk Kashembe, Simba ilishinda mataji mawili ya Ligi Kuu na moja la Shirikisho Tanzania.
Pia, timu ya wanawake ya Simba ‘Simba Queens’ ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.