KOCHA mpya wa Ceasiaa Queens, Ezekiel Chobanka amesema anahitaji nyota wapya wanne ili kukiongezea nguvu kikosi hicho.
Chobanka alisajiliwa msimu huu akitokea Alliance Girls ambako alidumu kwa takriban misimu saba akiibua nyota kama Aisha Masaka anayekipiga Brighton ya Uingereza, Aisha Mnunka (Simba Queens).
Akizungumza na Mwanaspoti, Chobanka alisema ni ngumu kwa kocha kuwafahamu wachezaji kwenye wiki za kwanza lakini kwake imekuwa rahisi kutokana na kuwafahamu kitambo kidogo.
Chobanka alisema anaifahamu Ceasiaa muda kidogo na kuna mapungufu kwenye maeneo matatu yaani kiungo, mabeki na mshambuliaji mmoja akitaka kuongezewa wapya dirisha hili.
“Pamoja na ubora wa timu lakini kuna baadhi ya mapungufu, nimeongea na viongozi na kuwapa ripoti nahitaji kiungo wa chini, mshambuliaji beki wa kati na pembeni mmoja,” alisema Chobanka.