Kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa kunawatia wasiwasi Wachad – DW – 23.12.2024

Kikosi cha jeshi la Ufaransa nchini Chad ambacho kimeanza kuondoka kilikuwa na wanajeshi zaidi ya elfu moja. Kuondoka kwa wanajeshi hao kumefuatia hatua ya serikali ya Ndjamena kusitisha mkataba wa kiulinzi na Ufaransa.

Aidhaa, hatua hiyo inaendelea kuibua wimbi la wasiwasi miongoni mwa Wachad walioajiriwa katika huduma za vituo vya kijeshi vya Ufaransa vilivyoanzishwa nchini humo kwa miongo kadhaa sasa. Raia wa Chad wapatao mia tano hutegemea mishahara inayolipwa na Ufaransa ili kukidhi mahitaji ya familia zao.

Kwa miaka miwili, Mohamed, anafanya kwenye kambi ya kijeshi ya Sergent-Chef Adji Kosseï  inayomilikiwa na jeshi la Ufaransa huko N’Djamena. Amesema amesikitishwa na hatua hiyo ya ghafla.

“Kwetu sisi, ni mshtuko. Tulijenga maisha yetu hapa, na sasa ni tishio kubwa kwa maisha yetu. Wafaransa walikuwa washirika wetu, na kuondoka kwao kunatupa wasiwasi mkubwa. Tunajiuliza tuanzie wapi ? na ni jinsi gani tunatafuta kazi nyingine ya kutunza familia zetu.”, alisema Mohamed.

“Hakuna ajira nyingi hapa nchini”

Hadi sasa Uafaransa inawanajeshi mia saba nchini Senegal na Gabon, mia sita nchini Cote d'Ivoire na zaidi ya elfu moja huko Chad
Hadi sasa Uafaransa inawanajeshi mia saba nchini Senegal na Gabon, mia sita nchini Cote d’Ivoire na zaidi ya elfu moja huko ChadPicha: Stanislas Poyet/AFP

Kwa upande wake Sandrine ambaye ni mama wa watoto watatu, mumewe anafanya kazi katika idara ya vifaa ya kituo  kikingine cha kijeshi cha Ufaransa huko N’Djamena. Sandrine anatoa wito kwa serikali ya Chad kutafuta suluhu kwa Wachad hao ambao watanyimwa kazi baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini humo.

“Endapo kambi hii itafungwa sijui tutapambana vipi na maisha, hakuna ajira nyingi hapa nchini, hatupingani na uamuzi huu lakini ni lazima serikali isimamie kutafuta ajira kwa wale wote ambao watapoteza ajira kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa”.

DW haikuweza kuwasiliana na mamlaka ya Chad ili kutoa maoni juu ya wasiwasi huu wa raia wake.  Wachadi walioajiriwa na kikosi cha jeshi la Ufaransa ni pamoja na mawakala wanaohusika na usafirishaji wa vifaa na upishi. Hospitali katika kituo cha kijeshi cha Ufaransa huko N’Djamena pia inatoa huduma bora ya afya kwa idadi ya watu.

Kulingana na afisa mmoja wa kikosi cha Ufaransa nchini humo ni kwamba Wachad hao watafutwa kazi kwa mujibu wa sheria za ndani za Chad.

Hatua ya kusitishwa mkataba wa ulinzi na Ufaransa ilichukuliwa kwa msangao mkubwa na raia wa Chad. Hata hivyo serikali ya Chad haijatoa sababu ya wazi ya hatua yake hiyo.

Related Posts