NANOFILTER MKOMBOZI WA MAJI SAFI NA SALAMA TANZANIA

NA. MWANDISHI WETU

Teknolojia ya kuchuja maji ya “NANOFILTER” imeendelea  kuimarisha jitihada za usafi wa mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama ili kuendelea kuhudumia jamii kwa kuwapata maji safi na salama ya kunywa hususani wanafunzi waliopo shule za Msingi na Sekondari nchini.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu kwa kushirikiana  na shirika la ActionAid Tanzania (AATZ), imeratibu ziara ya kikazi ya maafisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa “TAMISEMI”, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, Wizara ya Maji, Wizara ya Fedha,  wametembelea eneo la Ngongali TASS  (Tanzania Adventist Secondary School) iliyopo wilayani Arumeru Mkoani Arusha na makao makuu ya “NANOFILTER” Jijini Arusha, tarehe 22 Disemba, 2024.

Lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuongeza ufahamu juu ya uvumbuzi wa teknolojia hiyo ya “NANOFILTER” na  Matumizi yake.

Katika ziara hiyo wamepata fursa ya  kujionea teknolojia ya kuchuja maji ili kupata maji safi na salama ya kunywa, kupitia mvumbuzi wa teknolojia hiyo, Profesa Askwar Hilonga, kutoka Taasisi ya Nelson Mandela.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Profesa Askwar Hilonga amesema kuwa teknolojia ya kuchuja maji lengo lake kuu ni kukabiliana na magonjwa yatokanayo na bakteria waliopo kwenye maji na kemikali hatarishi katika maji ya kunywa.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la ActionAid, Profesa Oskar Mkasa alipongeza na kumshukuru Profesa Askwar Hilonga kwa elimu aliyoitoa kwa washiriki wa ziara hiyo,  na jitihada aliyoitumia katika kuvumbua mashine hizo, na kusisitiza kuwa, lengo la ziara hiyo pamoja na kujifunza watahakikisha, teknolojia hiyo wanaiwezesha  kuzifikia  shule za msingi na sekondari elfu ishirini na Tina (29000) Tanzania Bara, shule elfu moja na mia mbili (1200) kwa upande wa Zanzibar, ili kuziwezesha kupata maji safi na salama.

Related Posts