Handeni. Watu wanane wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori na Toyota Coaster iliyotokea Kijiji cha Michungwani, Kata ya Segera wilayani Handeni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amethibitisha kutokea kwa ajali leo Desemba 24, 2024, saa 11:00 asubuhi, Kitongoji cha Kwachuma, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni, Barabara Kuu ya Segera-Chalinze.
Amewataja majeruhi katika ajali hiyo ni Godlisen Minja (20) mfanyabiashara na mkazi wa Mabibo Dar es Salaam, Riziki Mboya (28) dereva na mkazi wa Njiapanda Moshi, Lina Swai (25) mfanyabiashara, Gospan Lema (24) fundi umeme na mkazi wa Temeke, Dar es Salaam.
Wengine ni Loyce James (27) mkazi wa Buguruni Dar es Salaam, Lucy Urio (24) mkazi wa Dar es Salaam, dereva wa lori Yona Madandi (35), mkazi wa Goba Dar es Salaam na utingo Samweli Hossen (24), mkazi wa Dar es Salaam.
Kamanda Mchunguzi amesema ajali hiyo imehusisha lori mali ya Kampuni ya Starling Gulf Trading likitokea Tanga kuelekea Dar es Salaam na basi dogo aina ya Toyota Coaster, mali ya Naman Joel Mkumbo likitokea Dar es Salaam kuelekea Kilimanjaro.
Endelea kufuatilia Mwananchi.