BoT yasisitiza marufuku makato katika malipo ya kadi

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imepigilia msumari katazo lake la kutoza ada au gharama za ziada katika miamala inayofanywa kwa kutumia mashine za malipo ya wafanyabiashara (POS) huku ikiwataka wananchi kutoa taarifa watakapokutana na hali hiyo.

BoT imetoa tangazo hilo jana Desemba 23, 2024 ikiwa ni siku 160 tangu katazo hili litolewe  Julai 16, 2024 huku ikieleza kuwa, hilo linafanyika baada ya kuwapo kwa upuuzaji wa agizo lililotolewa awali.    

Kwa mujibu wa tangazo hilo la BoT, hiyo ni moja ya hatua iliyochukuliwa ili kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali nchini.

“Hatua hii ililenga kuhakikisha kuwa malipo yanayofanywa kwa kutumia mashine za malipo za wafanyabiashara (Point of Sale – POS) ni bure kabisa kwa watumiaji wa kadi,” inasema taarifa hiyo.

“Kufuatia hili inawakumbusha wananchi kuwa malipo yanayofanywa kwa kutumia kadi za benki (debit, credit au prepaid) kwenye mashine yoyote ya POS hayapaswi kutozwa ada.

“Wafanyabiashara wote wamekatazwa kutoza ada au gharama za ziada kwa miamala inayofanywa kwa mashine za POS. Benki Kuu inawahimiza Watanzania kuendelea kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali kwa kuwa ni njia salama, rahisi na yenye gharama nafuu ya kukamilisha miamala,” inasema taarifa hiyo.

Matumizi ya mifumo ya kidijitali, ikiwamo kadi za malipo, huchangia kujenga uchumi wenye matumizi kidogo ya pesa taslimu na pia huleta faida kama usalama, uwazi na urahisi wa matumizi.

“Iwapo mlipaji utatakiwa kulipa ada au gharama za ziada unapotumia mashine yoyote ya POS, tafadhali toa taarifa kwa benki yako au wasiliana na Dawati la Malalamiko la Wateja wa Benki Kuu ya Tanzania kupitia.”

Kwa mujibu wa mwongozo kuhusu ada na tozo kwa watoa huduma ndogo za fedha, 2024 kifungu cha 19, kinakataza benki au taasisi ya kifedha na mfanyabiashara kutoza ada na tozo kwa watu wanaofanya malipo kwa wafanyabiashara kupitia kadi.

“Kifungu kidogo cha pili katika mwongozo huo kinasema bila kuathiri mwongozo wa 19 (1), benki itaweka vikwazo kwa wafanyabiashara endapo watatoza ada ya ziada kwa malipo ya kidijitali ya wafanyabiashara.

“19(3) Bila kuathiri mwongozo wa 19 (1) na (2), benki au taasisi ya kifedha itafanya yafuatayo, (a) kutunza orodha ya wafanyabiashara wasiofuata masharti kulingana na mwongozo wa 19 (1), (b) kuwasilisha taarifa hizo kwenye daftari kuu la taarifa na (c) kutumia taarifa hizo kama sehemu ya uhakiki wa kina na mapitio ya mikataba,” unaeleza mwongozo huo.

Adhabu inayotajwa na mwongozo huo ni faini au adhabu isiyozidi Sh20 milioni za Kitanzania kwa taasisi ya fedha itakayoshindwa kuzingatia matakwa ya miongozo hii.

Wakati miongozo ikisema hivyo, Mtaalamu wa Biashara na Uchumi, Dk Donath Olomi amesema moja ya sababu ya watu kukimbia malipo ya huduma kwa njia ya kielektroniki ni kukimbia makato.

Amesema hali hiyo inafanya watu wapende kutoa hela benki na kutembea nazo mkononi ili waweze kulipa huduma inapohitajika.

“Pamoja na kupunguza tozo ila ukitoa hela benki ukalipa kwa kutumia wakala, makato bado ni makubwa sana mtu anaona bora atumie hela yake akalipe huduma, sasa kuondoa hizi tozo utasaidia sana kufanikisha malipo ya huduma kielektroniki

Related Posts