Dar es Salaam. Mfanyabiashara Vicent Masawe (36) aliyekuwa bwana harusi, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili yanayomkabili likiwamo la wizi wa gari.
Masawe amefikishwa mahakamani leo Jumanne Desemba 24, 2024 kwa tuhuma za wizi wa gari aina ya Toyota Ractis lenye thamani ya Sh15milioni aliyoazimwa na Silvester Massawe kwa ajili ya kulitumia katika harusi yake, lakini hakulirejesha na kujipatia Sh3 milioni kwa njia ya udanganyifu.
Aidha, Masawe ambaye ni mkazi wa Kigamboni amefikishwa mahakamani hapo na kusomewa kesi ya jinai na Wakili wa Serikali Frank Rimoy mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.
Endelea kufutalilia mitandao ya kijamii.