Chombo cha anga za juu chalikaribia jua

Chombo cha anga za juu cha Shirika la Anga la Marekani (Nasa), Parker Solar Probe (PSP) kimeendelea kulikaribia jua hatua inayotaja kuweka historia ya vyombo vya anga kufikia hatua hiyo.

PSP ni chombo cha angani cha Nasa kilichozinduliwa mwaka 2018 kwa lengo la kuchunguza tabaka la nje la jua (corona ya Jua), ambayo ni anga ya nje ya Jua kilisafiri nje yay a anga la dunia kikistahimili joto na mionzi mikali.

Lengo la kurushwa kwa chombo hicho ni kuelewa vyema upepo wa jua (solar wind) na hali ya anga za juu za anga za Jua (space weather), ambazo zinaweza kuathiri setilaiti, mifumo ya mawasiliano, na gridi za umeme duniani.

Pia kinalenga kujibu maswali ya msingi kuhusu fizikia ya jua, kama vile kwa nini corona ya Jua ni ya moto zaidi kuliko uso wa jua.

Dk Nicola Fox, mkuu wa sayansi katika Nasa, aliiambia BBC kuwa: “Kwa karne nyingi, watu wamejifunza kuhusu jua, lakini hupati uzoefu wa mazingira ya mahali hadi utakapotembelea.”

Chombo hicho kitakaribia hadi mara 9.86 ya miale ya jua karibu kilomita milioni 6.9 au maili milioni 4.3 kutoka katikati ya Jua, kuwa karibu zaidi na Jua kuliko chombo chochote kilichowahi kufika.

Related Posts