Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amewataka wananchi mjini humo wenye watoto wanaosoma kukumbuka kutunza akiba ya fedha kwa ajili ya watoto kwenda shuleni Januari badala ya kumaliza bajeti kwa ajili ya sikukukuu
Mpete ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini hii leo kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka ambapo amesema ni wajibu wa wazazi kukumbuka kutenga bajeti kwa ajili ya watoto kwenda shuleni wakati zikitengwa bajeti kwa ajili ya sikukuu ili kufanikisha wanafunzi kwenda shuleni na kuwahi muhula wa masomo.
“Niwasihi na kuwaomba wazazi wakumbuke kwamba inapofika Januari wapo watoto amabo wataanza darasa la kwanza na wengine wanakwenda kuanza kidato cha kwanza sasa ni wakati pia wa kufanya maandalizi ili kuhakikisha watoto wote wanaotakiwa kwenda sekondari au shule ya msingi wanakwenda kwa hiyo niwasihi tunapofanya bajeti za maandalizi haya ya sherehe tuweke pia bajeti za kuhakikisha watoto wanakwenda shuleni”amesema Mpete
Amesema kutokana na mkakati wa halmashauri iliyojiwekea kwenye sekta ya elimu pamoja na serikali kuimarisha miunombinu wanao wajibu wa kuhakikisha watoto wote waliofanikiwa kuandikishwa wanafika shuleni kwa wakati ambapo hatua kali za kisheria zitakwena kuhukuliwa kwa wazazi watakaokwenda kinyume na utaratibu uliowekwa.