Mwenyekiti
Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs
Mwambegele, akikagua mafunzo kwa vitendo ya Waandishi wasaidizi na
waendesha vifaa vya biometriki (BVR) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Mbeya mkoani Mbeya leo Desemba 24, 2024. Mkoa wa Mbeya, Iringa na
Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma inataraji kuanza uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Desemba 27 mwaka huu hadi Januari 02,
2025. (Picha na INEC).