Rais Mwinyi ahamasisha jezi ya timu ya taifa ZNZ ivaliwe

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi ametoa punguzo la Jezi za Timu ya Taifa ya Zanzibar ambazo awali jezi hizo zilikua zikiuzwa kwa Tsh 40,000 na kutaka ziuzwe kwa 25,000

Ambapo kwenye taarifa kwa Umma iliotolewa ikulu na Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais Ikulu Charles Hilary ilieleza kua katika kuelekea Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar Ofisi ya Rais, Ikulu Zanzibar, inawaarifu wananchi wote nawapenda michezo kwamba katika sherehe za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,michuano ya Mapinduzi Cup itashirikisha timu za kandada za mataifa mbalimbali ambazo zimealikwa ikiwemo timu ya sokaya Zanzibar Heroes Tuoneshe uzałendo kwa kuujaza Uwanja wa Gombani kwa jezi za timu yetu ya Zanzibar Heroes

” Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa punguzo la bei kwa mashabiki wote ili kuvaa jezi ya timu ya Taifa, Zanzibar Heroes. Jezi hizo hivi sasa zinauzwa kwa shilingi 25,000 badala ya shilingi 40,000 Punguzo hilo la shilingi 15,000 limegharamiwa na Rais, Dkt.Mwinyi.

Onesha uzalendo kwa kuishangilia Zanzibar Heroes ili ibakishe Mapinduzi Cup nyumbani”

Related Posts