Ndege ya Azerbaijan iliyokuwa imebeba abiria 67 imeanguka karibu na mji wa Aktau nchini Kazakhstan na kusababisha vifo vya watu 38.
Ndege hiyo ilianguka jana, Desemba 25, 2024 na watu 29 waliokolewa, wakiwemo watoto wawili waliokuwa kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Naibu Waziri Mkuu wa Kazakhstan, Kanat Bozumbayev, amesema manusura 11 kati yao wapo walio na hali mbaya na wamepelekwa hospitalini, kati yao hakuna raia wa Kazakhstan.
“Miili iko katika hali mbaya, imeungua sana, yote imekusanywa. Sasa itakuwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na utambuzi utafanyika.” amesema Bozumbayev.
Kwa mujibu wa Shirika Ndege la Azerbaijan, ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Azerbaijan, Baku kuelekea Grozny eneo la Chechnya nchini Urusi, ililazimika kutua kwa dharura umbali wa kilomita tatu kutoka Aktau.
Endeleakufuatilia Mwananchi.