Hivi ndivyo mabibi na mababu walivyopanga uzazi

Unajua kama zamani licha ya kutokuwapo kwa vidonge na njia za kisasa za upangaji uzazi, bado wazee wetu hawakuwa nyuma katika kupanga uzazi?

Nini walichokuwa wakifanya?Jibu unalo hapa. Ni hivi kilichokuwa kikifanyika ni baba kulazimika kukaa mbali na mkewe kwa miaka mitatu kutoka siku mama alipojifungua.

Ofisa Elimu wa Kijiji cha Makumbusho, Wilhelmina Joseph, anasema katika kulifanikisha hilo, katika makabila mengi, baba alijenga nyumba ya pili na kukaa huko peke yake bila kuwa na uhusiano wa kindoa.

Hata hivyo, anasema inapotokea baba kuzidiwa, aliruhusiwa kuwa na mwanamke mwingine kwa muda huo.

Mwanamke huyo ilikuwa anamtafuta mwenyewe au anatafutiwa na mke wake na baada ya miaka mitatu waliachana.

“Malengo ya kufanya hivi ilikuwa ni kumpa mama nafasi ya kurudisha afya yake, baada ya pilikapilika za ujauzito kwa miezi tisa.Lakini kubwa kumpa nafasi ya kulea mtoto na kuepuka kumpa mimba nyingine, anasema Wilhelmina.

Anasema baba anapokuwa nyumba ya nje, mama yeye anabaki na mtoto ndani ya nyumba kubwa, na kadri anavyozidi kuzaa watoto wengine anaendelea kulala nao huko.

Inapofika muda wa kufanya tendo la ndoa na baba, Wilhelmina anasema mama alitumia muda wa kumpelekea chakula na kuweza kumaliza mambo yote huko, hivyo hakuna mtoto aliyekuwa akijua nini kinaendelea.

Related Posts