Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan anawajali watu wenye Mahitaji Maalum kwani ameweka mazingira mazuri ya kuwalinda na kuwapatia huduma muhimu hasa katika Makao ya Watoto na Makazi ya Wazee yaliyopo nchini.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema hayo Zanzibar Desemba 26, 2024 wakati akitoa zawadi za Sikukuu ya Christmas na Mwaka kwa niaba ya Rais Samia katika Makazi ya wazee Zanzibar.
“Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kawaida yake inapofika msimu wa sikukuu kama hizi kutoa zawadi Kwa watoto, wazee na wananchi ili waweze kufurahia Kwa pamoja, na leo ameona ni vema kuwafikia watu wa Zanzibar” amesema Naibu Waziri Mwanaidi.
Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri Mwananidi amewataka wananchi kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuwajali na wenye mahitaji Maalum ikiwa pamoja na kuwapa msaada na mahitaji mbalimbali.