Taifa Stars uhakika Afcon, Guinea yaangukia pua CAF

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imetupilia mbali rufaa ya Guinea dhidi ya Tanzania na hivyo kuipa uhakika Taifa Stars kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) nchini Morocco.

Guinea ilikata rufaa hiyo baada ya mchezo namba 143 wa kuwania kufuzu Afcon baina yao na Tanzania uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Novemba 19, 2024 ikiitaka kamati ya nidhamu ya CAF kuiondoa Tanzania katika fainali za Afcon 2025 wakidai ilifanya kosa la kufoji kinyume na kanuni.

Kwa mujibu wa rufaa hiyo, Guinea ilidai kuwa mchezaji Ibrahim Ame wa Tanzania aliyeingia kipindi cha pili kwenye mechi hiyo ambayo Tanzania iliibuka na ushindi wa bao 1-0 alikuwa na namba tofauti kwenye jezi kulinganisha na ile iliyopo kwenye fomu ya orodha ya wachezaji wa kutumika kwenye mechi hiyo.

Guinea waliiomba kamati ya nidhamu ya CAF kuiengua Tanzania na kisha nafasi ya kucheza Afcon 2025 wapewe wao.

Hata hivyo kamati ya nidhamu ya CAF iliyoketi Desemba 19, mwaka huu imeamua kuwa matokeo ya mchezo huo yabaki kama ilivyokuwa na Tanzania ibaki na haki ya kushiriki Afcon 2025.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Guinea (Feguifoot) leo imeeleza kuwa rufaa yao imeangukia pua.

“Kamati ya nidhamu ya CAF imekubali kwamba uhifadhi wa ushahidi uliofanywa na Shirikisho la Soka Guinea wakati wa mechi namba 143, Tanzania vs Guinea unakubalika katika fomu.

“Hata hivyo umekataliwa kwa vile hakuna hoja ya msingi,” imefafanua taarifa hiyo ya Shirikisho la Soka Guinea.

Mapema baada ya kusambaa kwa taarifa za Guinea kukata rufaa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliwatoa wasiwasi Watanzania kwa kufafanua kuwa taratibu zote zilifuatwa katika kumtumia Ibrahim Ame kwenye mchezo huo.

“Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshangazwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu uhalali wa mchezaji Muhamed Ame kuchezea timu ya Taifa (Taifa

“Tunapenda kufahamisha umma kuwa Ame ni miongoni wa wachezaji 23 waliokuwa wameorodheshwa kwa ajili ya mechi dhidi ya Guinea. Kabla ya mechi hiyo, wachezaji wa Stars walikaguliwa na timu pinzani pamoja na Kamishna ambapo waliruhusiwa kucheza.

“Mechi hiyo ya mchujo ya Afcon ilichezwa Dar es Salaam ambapo Stars ilishinda bao 1-0, hivyo kufuzu kucheza fainali. TFF haina taarifa yoyote kutoka Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuwa ushiriki wa Ame katika mechi hiyo haukuwa halali.

“Hivyo, taarifa hizo za mitandaoni zisiwazuie Watanzania kuendelea kushangilia ushindi wa

Taifa Stars,” ilifafanua taarifa hiyo ya TFF.

Related Posts