Watano wahofiwa kufariki ajali ya basi, Noah Rombo

Rombo. Watu zaidi ya watano wanahofiwa kufariki dunia katika Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro baada ya basi la abiria Kampuni ya Ngassero kugongana na basi dogo la abiria aina ya Toyota Noah eneo la Tarakea wilayani humo.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Desemba 26, 2024 Mkuu wa Wilaya hiyo, Raymond Mwangwala ambaye yuko njiani kuelekea eneo la tukio amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema akifika eneo la tukio atatoa taarifa kamili.

Wiki hii takribani ajali tatu zimetokea mikoa ya kaskazini ya Tanga na Kilimanjaro na kusababisha vifo vya watu jumla 21.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.

Related Posts