Asili ya maneno kuchimba, dawa, kukata gogo

Imezoeleka kwa watu hasa wasafiri kutumia tafsida wanapotaka kwenda haja kubwa au ndogo.  Maneno maarufu ni ‘kukata gogo’ kwa haja kubwa huku wanaoenda haja ndogo wakisema ‘wanakwenda kuchimba dawa’.

Unajua maneno yalitokea wapi? Kuna mahali yalianzia.

Ofisa Elimu wa Kijiji cha Makumbusho, Wilhelmina Joseph, anasema zamani jamii nyingi za makabila ya Kitanzania, zilikuwa zinajenga nyumba lakini hazikuwa na vyoo kama ilivyo sasa.

Kutokana na hilo, walipokuwa wakishikwa na haja walizoea kwenda kujisaidia vichakani au msituni.

Hata hivyo, ilipotokea kwa mfano, baba anataka kwenda kukidhi haja na anataka kumuaga mama mbele ya watoto, kuna ujanja wa kimaneno uliotumika ili kuwaficha watoto waliokuwa jirani.

Kwa kawaida, baba angeweza kusema kuwa anakwenda kukata gogo kama ni haja kubwa. Na ikiwa ni haja ndogo, alisema anakwenda kuchimba dawa.

Wilhelmina anasema  watoto walizidi kuaminishwa ukweli wa baba kwenda kukata gogo,  kwani ni kweli baba alikuwa akitoka huko lazima arudi na gogo  au magome na majani yoyote yanayoonyesha kuwa ni dawa kama alikwenda kwa minajili ya kukidhi haja ndogo.

Haya sasa kwa wale wasafiri mnapofika njiani na kusikia tutasimama hapa kuchimba dawa  na kula dakika kumi; eleweni kuwa mnarejea misemo iliyotumika miaka mingi iliyopita!

Tofauti na zamani wazee walipokata magogo na kuchimba dawa misituni, leo dawa au gogo linaweza kuchimbwa hata kwa mtu akiwa amekaa na pengine akichezea simu.

Ni hivi magogo na dawa vinachimbwa ndani ya majengo mazuri pasipo hofu ya wadudu au wanyama wanaoweza kuharibu raha ya ‘kukata gogo.’

Related Posts