Mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA yatakuwa na michezo mingi, ikiwemo mpira wa kikapu, bao, karata, drafti, msusi mwenye kasi zaidi, mbio za baiskeli, Netball, wavu, PS Game, mchezo wa kufukuza kuku, kushindana kula, pull table na muziki.
Michezo mingine, kama vile mchezo wa bao, karata, drafti, na msusi mwenye kasi zaidi tayari imezinduliwa na mashindano hayo yatafikia tamati siku ya Desemba 31, 2024.
Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro
Lengo la Mashindano
Mratibu Jackline Isaro amesema kuwa lengo kuu la mashindano haya ni kufufua michezo mkoani Shinyanga na kutoa fursa kwa wachezaji na wadau wa michezo kuonyesha vipaji vyao.
Isaro amesisitiza kuwa michezo ni muhimu kwa jamii kwa sababu inachangia afya, furaha, na pia ajira.
“Lengo la michezo hii ni kuonesha vipaji vya vijana wetu mkoani Shinyanga, na tunaamini kupitia mashindano haya tutapata wachezaji bora ambao watakuwa na nafasi ya kuendelezwa. Tunajua pia kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anahimiza michezo, na kupitia mashindano haya, tunatarajia kukuza michezo na vipaji katika mkoa wetu,” amesema Isaro.
Zawadi kwa Washindi
Mashindano haya yatatoa zawadi nono kwa washindi, ikiwa ni pamoja na fedha taslimu, ng’ombe, mchele na kreti za soda. Kwa mfano: Mchezo wa mpira wa miguu kati ya Upongoji Sports Club na Upongoji Stars: Mshindi atapata shilingi milioni moja, ng’ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 10 za soda na Mshindi wa pili atapata shilingi 500,000/=, ng’ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 10 za soda.
Mchezo wa Mabingwa wa Wilaya (Rangers FC vs Ngokolo FC), Mshindi atapata shilingi 500,000/=, ng’ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 10 za soda, Mshindi wa pili atapata shilingi 300,000/=, ng’ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 10 za soda.
Mchezo kati ya Bodaboda FC vs Bajaji FC, Mshindi atapata shilingi 500,000/=, ng’ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 7 za soda na Mshindi wa pili atapata shilingi 300,000/=, ng’ombe mmoja, mchele kilo 100, na kreti 7 za soda.
Pia, mashindano ya mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake yatakuwa na zawadi kwa washindi kutoka nafasi ya kwanza hadi ya kumi.
Washindi wa michezo mingine kama bao, karata, drafti, na msusi mwenye kasi zaidi pia watapata zawadi ya shilingi 100,000/= kila mmoja.
Kwa upande wa Mpira wa pete, mshindi wa kwanza atapata shilingi 500,000=, kreti 7 za soda, na mchele kilo 50, huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi 300,000/=, mchele kilo 50, na kreti 7 za soda.
Zaidi ya hayo, zawadi za shilingi 100,000/= zitatolewa kwa washindi wa pull table, huku mashindano ya kufukuza kuku na kushindana kula yatatoa zawadi za kuku na shilingi 20,000/= kwa mshindi upande wa wanawake na wanaume.
Jackline Isaro akizungumza na waandishi wa habari
Mratibu Jackline Isaro ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo hii.
Amesisitiza kuwa hakutakuwa na kiingilio kwa michezo yote, hivyo ni fursa nzuri kwa watu wa Shinyanga kuungana pamoja na kusherehekea mapumziko ya mwaka kwa njia ya michezo.
“Tunawaalika Wanashinyanga wote kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo hii ambayo itafanyika rasmi Desemba 31, 2024 kuanzia asubuhi katika uwanja wa CCM Kambarage. Hakutakuwa na kiingilio cha aina yoyote,” amesema Isaro.
Nao Washiriki wa bonanza hilo akiwemo Mohamed Juma, Ngassa Swaganya na James Edward wameonyesha furaha na shauku kubwa kushiriki bonanza hilo na wakisema ni fursa nzuri kuonesha vipaji vyao.
Mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA ni fursa muhimu kwa kuendeleza michezo mkoani Shinyanga na kutangaza vipaji vya vijana.
Pamoja na burudani ya michezo, zawadi za kuvutia zinatoa motisha kwa washiriki na kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za kijamii zinazochangia maendeleo ya afya na ustawi wa watu.
Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro akielezea kuhusu mashindano hayo. Picha na Kadama Malunde
Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro akiwa na viongozi wa timu zitakazoshiriki katika mashindano ya mpira wa kikapu
Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro (kushoto) akikabidhi jezi kwa moja ya timu zitakazoshiriki katika mashindano ya mpira wa kikapu Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro (kushoto) akikabidhi jezi kwa moja ya timu zitakazoshiriki katika mashindano ya mpira wa kikapu
Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro (kushoto) akikabidhi jezi kwa moja ya timu zitakazoshiriki katika mashindano ya mpira wa kikapu
Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro (kushoto) akikabidhi jezi kwa moja ya timu zitakazoshiriki katika mashindano ya mpira wa kikapu
Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA, Jackline Isaro (kushoto) akikabidhi jezi kwa moja ya timu zitakazoshiriki katika mashindano ya mpira wa kikapu
Mwenyekiti wa Timu ya Bodaboda FC, Mohamed Juma akielezea namna walivyojipanga kushiriki mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA
Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Shinyanga, Ngassa Swaganya akielezea namna walivyojipanga kushiriki mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA
Mchezaji wa Basket Ball , James Edward akielezea namna walivyojipanga kushiriki mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA