Hasnath: Kiarabu noma, ila tunaelewana

WINGA wa FC Masar inayoshiriki Ligi ya Wanawake nchini Misri, Hasnath Ubamba amesema lugha ya Kiarabu ambayo ndio inatumika nchini humo ikiwamo mazoezini ni ngumu lakini anapata msaada kutoka kwa nyota wenzake wa Afrika Mashariki.

Nyota huyo ni msimu wake wa kwanza kucheza ligi hiyo akitokea Fountain Gate Princess ya Tanzania kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Ubamba alisema hayo wakati akijibu swali la shabiki yake akiwa mubashara kwenye mtandao wa Tiktok.

“Lugha ni ngumu lakini tunawasaliana vizuri uwanjani ila kuna muda kocha akizungumza Kiarabu sielewi hivyo kuna wachezaji wenzangu wawili wanajua hivyo wananitafsiria,” alisema.

“Ni kigumu sana nina karibia mwaka sasa lakini sijui maneno wanayoongea na sitaki kufahamu mengine yatupite tu ila mtu akiomba pasi unaelewa.”

Winga huyo amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho akitumika nafasi mbalimbali kama kiungo mshambuliaji.

Related Posts