M-Bet, HaloPesa waanza kumwaga zawadi za washindi wa kampeni ya amsha amsha

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Halotel kupitia HaloPesa zimezawadia washindi wa kwanza wa kampeni ya Amsha Amsha zawadi mbalimbali.

Meneja Masoko wa M-Bet, Levis Paul amewataja washindi hao kuwa ni Ramadhan Mussa wa Dodoma na Greta Godfrey wa Dar es Salaam ambao wameshinda simu janja za mkononi aina ya Samsung A-series zenye thamani ya Sh500,000 kila mmoja.

Mbali ya zawadi za simu za mkononi, pia mkazi wa Songea, Vedasto Augustino ameshinda televisheni aina ya Hisense yenye thamani ya Sh1.2 millioni.

Washindi wote wamekwisha patiwa zawadi zao ambapo, wakazi wa Dodoma na Songea wametumiwa kupitia utaratibu waliouweka.

Pia, Daniel Dende, Njelekela Vitass, Petro Edward, Manase Ernest, Paschaali Paulo, Joseph Kishala, January John, Yolanda George, Amani Yohana, Patrick Oswaldi, Esha Ally na Paul Lamson walishinda fedha taslimu, Sh50,000 kila mmoja.

Wengine walishinda Sh50,000 ni, Alhaji Jabir, Frank Aidan, Amuri Hamisi, Yahaya Hamad, Siado Emmanuel, Rajab Chande, Kanisus Patrick, Mwasi Mwandito, Mashaka Kombo, Andrew Yohana na Saidi Mohamedi.

Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Levis Paul alisema kuwa wanajisikia fahari kuwazawadia washindi hao zawadi hizo na kuwaomba kuendelea kushiriki kampeni hiyo ili kuendelea kushinda zawadi mbalimbali.

“Natoa wito kwa mashabiki wa soka na HaloPesa, kubashiri kuanzia dau la Sh2,000 ili kuweza kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja zawadi ya fedha taslimu kwa washindi wawili kwa siku,” alisema Paul.

Paul alisema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwazawadia wateja wao ambapo pia wanaweza kushindia fedha kwa kubashiri matokeo ya mechi katika ligi mbalimbali duniani.

“Washindi wawili wa kila siku watajishindia Sh50,000, ambapo jumla ya Sh6,000,000 zimetengwa kwa kipindi hiki cha sikukuu, droo itafanyika kila mwisho wa wiki, ” alisema Paul.

Alisema kuwa mpaka sasa kuna televisheni saba ambazo zinasubiri washindi na kuwaomba mashabiki wa soka kuendelea kubashiri ili kushinda televisheni hizo na pia simu za kisasa za smartphone. Kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi mitatu.

Alifafanua kuwa shabiki wa soka au mteja wao anaweza kuingia kwenye droo kwa kujisajili kupitia tovuti, www.m-bet.co.tz, kuweka pesa kupitia HaloPesa, na kubeti kwa dau la kuanzia Sh2, 000 ili kuingia kwenye droo,” alisema.

Mwakilishi wa kampuni ya simu ya Halotel, Keneth Bernald Wello (kulia) akimkabidhi zawadi ya televisheni aina ya Hisense yenye thamani ya Sh1.2 millioni Vedasto Agustino ambaye ameshinda kupitia kampeni ya Amsha Amsha.


Mwakilishi wa kampuni ya simu ya Halotel mkoani Dodoma, Jovita Minga (kushoto) akimkabidhi Ramadhan Mussa zawadi ya simu janja ya mkononi (smartphone) aina ya Samsung a-series aliyoshinda kupitia kampeni ya Amsha Amsha.

Related Posts