MBUNGE MAVUNDE PAMOJA NA TAASISI YA DODOMA LEGENDS WATEMBELEA GEREZA KUU ISANGA DODOMA

▪️Washiriki Bonanza la Michezo na Askari Magereza

▪️Watoa misaada mbalimbali kwa wafungwa

▪️Wafanya ukarabati wa Jiko lq
chakula kwa Wafungwa wanawake

▪️Jeshi la Magereza lapongezwa kwa matumizi ya Nishati Safi

📍Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, ametembelea Gereza Kuu Isanga akiambatana na wadau wa maendeleo Dodoma, maarufu kama ‘Dodoma Legends’ jana Desemba 28, 2024 na kupokewa na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza (CP) Nicodemus Tenga kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania (CGP) Jeremiah Katungu.

Katika ziara hiyo CP Tenga amepokea zawadi za vitu mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma Mjini.

Kamishna Nicodemus Tenga amemshukuru Mhe. Mavunde pamoja na wadau alio ambatana nao kwa kuamua kutembelea Gereza la Isanga na kutoa zawadi mbalimbali kwaajili ya matumizi ya Wafungwa na Mahabusu huku akisema hiyo ndio namna bora ya ushirikishwaji wa jamii katika dhana ya Urekebu wa wafungwa.

Akitoa Salamu fupi,Mh. Mavunde aliwapongeza wanaKikundi cha Dodoma Legends kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kujenga mahusiano mema na pia kwa misaada mbalimbali waliyoiratibu kwa lengo la kuwashika mkono wafungwa katika Gereza la Isanga sambamba na ukarabati mkubwa walioufanya wa jiko la chakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na kuwataka kufanya zoezi hilo kuwa endelevu kwani linarudisha tabasamu kwa Wafungwa na Mahabusu waliopo Gerezani.

Mhe. Mavunde akiwa Gereza Isanga pamoja na mambo mengine alipata fursa ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo la Serikali kuhusu Matumizi ya Nishati safi ya kupikia Magerezani na kulipongeza Jeshi la Magereza kwa utekekezaji wa haraka wa maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan juu ya matumizi ya nishati safi.

Related Posts