CRDB YAKABIDHI GARI JIPYA KWA MSHINDI KAMPENI YA BENKI NI SIMBANKING

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB,Bw. Stephen Adili,akimkabidhi funguo za gari pamoja na vifaa mbalimbali Bw.Khamis Majala mara baada ya kuibuka mshindi katika kampeni yao ya Benki ni Simbanking hafla liyofanyika leo Disemba 30,2024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Benki ya CRDB imemkabidhi gari jipya Bw.Khamis Majala baada ya kuibuka mshindi katika kampeni yao ya Benki ni Simbanking ambaye amefanya miamala mingi kwenye simu yake ya mkononi katika kampeni iliyolenga kuhamasisha matumizi ya huduma za SimBanking.

Zawadi hiyo ya gari aina ya Nissan Duals inafanya kufikisha magari mengine manne ambayo yalishatolewa kwa wateja hao na hivyo kufikisha jumla ya magari matano Mpaka sasa ambayo wateja hao wa CRDB wamejishindia.

Akizungumza leo Disemba 30,2024 jijini Dodoma  kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hiyo Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB,Bw. Stephen Adili,amesema lengo la kutoa zawadi hiyo ni kuhamasisha wananchi kutumia simu za mkononi kufanya miamala.

Ametaja faida za kutumia simu za mkononi kufanya miamala kuwa husaidia kufanya miamala wakati wote, kuokoa muda wa kupanga foleni kupata huduma na kuongeza usalama wa fedha.

“Leo tuko hapa kutoa zawadi kwa mshindi wetu wa  gari ambayo imesajiliwa, kujazwa mafuta full  tank na bima ya mwaka mzima. Mwanzoni mwa mwaka tulianzisha kampeni ambayo lengo ni kuhakikisha watanzania wanapata uelewa wa kutosha kuhusu huduma za benki zinazopatikana katika simu za mkononi,”amesema Bw.Adili

Ameongeza kuwa :”Wananchi walipokea kampeni hiyo  kwa furaha ambayo imesaidia kuongeza miamala kwa asilimia 100 na watu wanaotumia simu za mikononi kwa huduma za kibenki.

Kwa mujibu wa Bw.Adili amesema kuwa  katika kampeni hiyo walipanga kutoa zawadi ya  magari matano ambapo manne wameshayatoa tayari kwa washuindi waliopatikana kupitia kampeni hiyo.

kwa upande wake Meneja wa Biashara Kanda ya Kati Bw. Andrew Mheziwa amesema hadi sasa malipo yote yanaweza kufanyika kwa njia ya simu.

“Leo hii tunahitimisha ambapo mshindi wetu atakabidhiwa gari kwa mshindi wetu kutoka Dodoma. niendelee kuwahamasisha wananchi kufungua akaunti za CRDB  ambazo zitasaidia kufanya miamala kidigitali,”amesema

Naye Mshindi wa gari Bw.Khamis Majala amesema anaishukuru benki ya CRDB kwa kupata zawadi hiyo huku akihamasisha wananchi kuendelea kufanya miamala kidigitali ili waweze kushinda zawadi mbalimbali.

“Mwanzo nilisikia tu ila sikuamini nilijua ni ya mchongo lakini baada ya kupigiwa simu kuwa nimeshinda ndo nikaamini kumbe ni kweli. Hivyo naomba wananchi waendelee kufanya miamala kupitiaCRDB ili waweze kushinda kama mimi,”amesema Bw.Majala

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB,Bw. Stephen Adili,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi gari kwa mshindi baada ya kuibuka mshindi katika kampeni yao ya Benki ni Simbanking iliyofanyika leo Disemba 30,2024 jijini Dodoma.

Meneja wa Biashara Kanda ya Kati Bw. Andrew Mheziwa,akizungumzia kampeni yao ya Benki ni Simbanking wakati wa hafla ya kukabidhi gari mshindi Bw.Khamis Majala mara baada ya kuibuka mshindi kupitia kampeni hiyo  leo Disemba 30,2024 jijini Dodoma.

 Mshindi wa Gari Bw.Khamis Majala,akielezea furaha yake mara baada ya kupata zawadi ya gari .

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB,Bw. Stephen Adili,akimkabidhi funguo za gari pamoja na vifaa mbalimbali Bw.Khamis Majala mara baada ya kuibuka mshindi katika kampeni yao ya Benki ni Simbanking hafla liyofanyika leo Disemba 30,2024 jijini Dodoma.

Related Posts