Jaji Werema afariki dunia – Mwanahalisi Online

 

ALIYEKUWA Mwanasheria Mkuu (AG) wa Serikali, Frederick Werema amefariki dunia leo, tarehe 30/12/2024 katika Hospital ya Muhimbili.

Taarifa za kifo chake zimetolewa leo na Salome Ntaro, ambaye ni Katibu Parokia ya Mt. Martha ambayo marehemu Werema alikuwa mwenyekiti wake.

Kwa mujibu wa Ntaro, taratibu za msiba huo zinaendelea kwa kushirikiana na ndugu pamoja na serikali.

Jaji Werema, alijiuzulu uanasheria mkuu wa Serikali, tarehe 16 Desemba, 2014 baada ya kuhusishwa na kashfa ya Esrow iliyosababisha mawaziri kadhaa kujiuzulu.

About The Author

Related Posts