Sasa unaweza ku-repost ‘status’ ya mtu mwingine WhatsApp

Mtandao wa WhatsApp umeendelea kuboresha baadhi ya huduma zake ambapo kwa sasa unatoa fursa kwa mtu mwingine ku-reposti status ya mtu mwingine bila kuipakua.

Awali ilikuwa haiwezekani kuposti status iliyowekwa na mtu mwingine bila kuipakua, ila mabadiliko hayo yanaruhusu kwa mtu aliyetajwa (mentioned) kui-reposti tena status hiyo bila kuipakua.

Huu ni mwendelezo wa maboresho ya kiteknolojia yanayofanywa na mtandao huo unaotumiwa na takribani watu bilioni 2.96

pia WhatsApp imefanya maboresho kadhaa hivi karibuni ili kuboresha matumizi ya watumiaji wake. Baadhi ya maboresho haya ni pamoja na:

  1. Uhariri wa Ujumbe: Watumiaji sasa wanaweza kuhariri ujumbe waliotuma ndani ya dakika 15 baada ya kutuma, ikiwa na maana ya kurekebisha makosa au kuongeza maelezo muhimu.
  1. Mwitikio kwa Ujumbe (Reactions): Watumiaji wanaweza kujibu ujumbe kwa kutumia emoji, kurahisisha mawasiliano na kutoa hisia zao bila kuandika maneno.
  1. Uwezo wa Wasimamizi wa Vikundi (Admin): Wasimamizi wa vikundi sasa wana uwezo wa kufuta ujumbe wowote ndani ya kikundi, kusaidia kudhibiti maudhui na kuhakikisha mazungumzo yanabaki kwenye mstari unaofaa.
  1. Maboresho ya WhatsApp Business: Kwa wafanyabiashara, WhatsApp Business imeboreshwa kuruhusu wateja kuona bidhaa na kufanya malipo moja kwa moja ndani ya mazungumzo, kurahisisha mchakato wa ununuzi mtandaoni.

Related Posts