Russia. Ukraine imewaachia wanajeshi 150 wa Russia iliyokuwa imewakamata kama wafungwa wa vita (POW) katika mapigano yanayoendelea kati ya mataifa hayo.
Wakati Ukraine ikifanya hivyo, Russia nayo imewaachia wanajeshi 200 wa Ukraine waliokuwa wamekwama nchini humo tangu Russia itangaze kuanza operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine mwezi Februari 2022.
Mabadilishano hayo ya wanajeshi 95 ambao ni wafungwa wa kivita kwa pande hizo yaliyoratibiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), yamefanyika jana Desemba 30, 2024.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imeandika kwenye akaunti yake ya Telegram kuwa mabadilishano hayo yamefanyika chini ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa wa kivita kati ya mataifa hayo.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, wanajeshi wote wa Russia waliokuwa wamekamatwa mateka nchini Ukraine wamepelekwa nchini Belarus, kwa ajili ya kupewa msaada wa kisaikolojia na kimatibabu sambamba na kukutanishwa na wapendwa wao waliotenganishwa nao kwa muda mrefu.
Pia imesema baada ya afya zao kurejea katika utimamu, wanajeshi hao watarejeshwa nchini Russia kwa ajili ya kukamilisha matibabu yao.
Mabadilishano hayo ya wafungwa wa kivita ni ya kwanza kufanyika tangu Oktoba mwaka huu pande hizo zilipobadilishana wafungwa wa kivita 95 kila upande.
Novemva 2024, Russia na Ukraine pia zilibadilishana maiti za wanajeshi wake waliouawa maeneo katika maeneo mbalimbali ya vita hiyo ambapo miili ya wanajeshi 563 wa Ukraine ilirejeshwa kutoka Russia huku huku Russia ikipokea miili ya wanajeshi wake 37 waliofariki kwenye uwanja wa mapigano nchini Ukraine.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amethibitisha kufanyika kwa mabadilishano hayo na kusema zaidi ya wa wanajeshi 200 Ukraine wamerejeshwa kutoka nchini Russia.
“Kurejeshwa kwa watu wetu kutoka kifungoni Russia ni habari njema kwetu sote. Leo ni moja ya zile siku ambazo timu yetu imefanikiwa kurejesha zaidi ya wanajeshi 189 wanarejeshwa kwenye makazi yao,” Zelenskyy aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Telegram.
Kabla ya mabadilishano hayo, Moscow imekuwa ikiituhumu Kiev kutochukua hatua zozote za kuwarejesha raia na wanajeshi wake ambao wanashikiliwa kifungoni nchini Russia.
Mapema Desemba mwaka huu, Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Binadamu nchini Russia, Tatyana Moskalkova aliachapisha orodha ya wanajeshi wa Ukraine wanaoshikiliwa nchini Russia huku akidai kuwa maofisa wa Ukraine hawafanyi jitihada zozote kuwarejesha kwenye familia zao.
“Zelensky haonyeshi nia ya kuwarejesha raia 630 wa Ukraine ambao wanashikiliwa nchini Russia. Kifupi ni kwamba amewatekeleza,” amesema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Hungary, Victor Orban alipotembelea Ukraine katikati mwa Desemba alipendekeza pande hizo kufanya mabadilishano ya wafungwa wa kivita ambapo alisema mazungumzo hayo yanatakiwa kuhusisha angalau wanajeshi 700 kila upande.
Hata hivyo, baadae alitoa taarifa kuwa Ukraine imetolea nje pendekezo hilo.
Mmoja wa wasaidizi wa Rais Volodymyr Zelensky ameibuka na kumuita Orban kuwa ni mjumbe mnafiki anayetumiwa na Vladimir Putin, huku akiongeza kuwa mtu wa aina hiyo hapaswi kuendekezwa kwa kile alichodai halengi kupatanisha pande hizo.
Hata hivyo, Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amesema Russia ilikuwa tayari kutekeleza pendekezo la Orban na kusema kuwa Russia ilifanya mazungumzo na Ubalozi wa Hungary nchini Ukraine ili kupata mwafaka wa suala hilo.
Katika hatua nyingine, Rais Vladimir Putin amesaini ameamuru wahamiaji wote kukamilisha taratibu za kupewa uraia ama kuondoka nchini humo kabla ya Aprili 30, 2025.
Amri hiyo ya Putin ni sehemu ya utekelezaji wa sheria inayokaza minyoyoro ya vigezo vya uhamiaji nchini Russia.
“Wageni na wasiokuwa na uraia wa Shirikisho la Russia, mnatakiwa kuondoka ndani ya Russia wenyewe kuanzia Januari Mosi hadi Aprili 30, 2025,” imesema amri hiyo.
Hata hivyo, Putin kupitia amri hiyo amesema kwa wanaohitaji kubaki na kuwa raia wa Russia wanaruhusiwa huku akiwataka kutimiza matakwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha taarifa zao za Kibaiometriki (Biometric data), kufanyiwa vipimo vya matumizi ya dawa za kulevya, magonjwa ya kuambukiza, HIV, na kufaulu mtihani wa kuzungumza lugha ya taifa hilo, Historia na somo la sheria za taifa hilo.
Pia amesema wanaohitaji kuwa raia wa Russia wanapaswa kulipa madeni wanayodaiwa na kuhakikisha wana nyaraka safi, hususan ni kazi rasmi na kibali cha ukazi.
Hata hivyo, Putin amesema wanaopewa nafasi ya upendeleo ni waliokubali kusaini mikataba ya kulitumikia Jeshi la Russia ambapo amesema watakaofanya hivyo hawatokumbana na fagio la kuwaondoa nchinu humo na kuwarejea walikotoka.
Sheria mpya ya kudhibiti uhamiaji haramu ilipitishwa mwaka 2024, nchini humo ambapo miongoni mwa malengo ya kupitishwa sheria hiyo ni pamoja na kudhibiti mwingiliano wa watu ndani ya Russia.
Kuanzia Februari 5, 2025, mamlaka nchini humo zitakuwa na mamlaka ya kumfukuza mtu yeyote ambaye siyo raua wa Russia kuishi na kufanya kazi nchini humo bila hata kupewa kibali na mahakama endapo atakuwa hana kibali cha kufanya hivyoz
Sheria hiyo pia ilianisha kuwa mtu yoyote anayepanga kuingia ama kuingiza mhamiaji haramu ndani ya Russia atakuwa ametenda uhalifu wa kiwango kikubwa nchini humo.
Miongoni mwa adhabu kwa atakayebaini kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria mpya ni pamoja na kutozwa fedha na kutaifishwa kwa kifaa ama mali iliyotumika kuingiza wahamiaji nchini humo.
Uamuzi huo ulichukuliwa siku chache baada ya shambulizi linalotajwa kuwa la Kigaidi lililofanyika Machi 2024, katika Ukumbi wa sherehe wa Crocus Jijini Moscow na kusababisha vifo vya watu 145 huku zaidi ya 500 wakijeruhiwa.
Shambulizi hilo lilimsukuma Rais Putin kuamuru kupitiwa upya kwa sera ya uamiaji nchini humo Juni 2024, alipokuwa akihutubia katika Jukwaa la Kimataifa ka Kiuchumi lililofanyika jijini St Petersburg.
“Hatuwezi kujisshaulisha kwamba hakuna tatizo,” alisema Putin huku akidokeza kuwa pamoja na taifa hilo kutegemea wafanyakazi kutoka nje lakini Russia inapaswa kuratibu vyema shughuli za uhamiaji.
Akipigilia msumari kauli hiyo ya Rais, Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amesema Russia inahamasisha wahamiaji wanaotafuta kazi nchini Russia huku akisisitiza kuwa wanapaswa kufuata sheria zote zinazohitajika kuwa mtumishi wa Umma ndani ya taifa hilo.