Serikali itaendelea kuunga mkono matamasha :Rais Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesema Serikali itaendelea kuunga Mkono Matamasha yenye Manufaa na tija kwa Ukuaji wa Uchumi wa nchi.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na Mamia ya Wananchi kwenye Tamasha la Kwanza la Vumba lililofanyika Viwanja vya Kizingo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Matamasha yanayowasaidia Watu wenye Mahitaji maalum,kulinda Silka ,Utamaduni na Maadili yanapaswa kuendelezwa kwa maslahi ya jamii na nchi.

Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Wizara ya Uchumi wa Buluu kwa Ubunifu na kuandaa tamasha hilo la Vumba alilolielezea litasaidia kukuza Uchumi wa ndani ya nchi na ameridhia lifanyike kila mwaka.

Rais Dk.Mwinyi ametumia Fursa hiyo kuwatakia Wananchi heri ya Mwaka Mpya wa 2025.

Mapema Rais Dk. Mwinyi alishuhudia Mashindano ya Ngalawa yaliyoandaliwa maalum kwa Tamasha hilo na hatimae kukabidhi zawadi kwa Washindi.

Hafla hiyo iliambatana na Ugawaji wa samaki aina ya Jodari kwa Wananchi na mitungi ya gesi kwa Watu wenye Mahitaji maalum.

Related Posts