Kamishna Jenerali Philippe Lazzarini alisisitiza kwamba hakuna sehemu na hakuna mtu katika Gaza ambaye amekuwa salama tangu vita vilipoanza Oktoba 2023.
“Mwaka unapoanza, tulipata taarifa za shambulio jingine kwenye Al Mawasi na makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa,” alisema. alisemaakiita hii “ukumbusho mwingine kwamba hakuna eneo la kibinadamu sembuse 'eneo salama'”.
Alionya kwamba “kila siku bila kusitishwa kwa mapigano kutaleta maafa zaidi.”
Vyombo vya habari vinashambuliwa
Tofauti, UNRWA alikumbuka kuwa mamlaka za Israel zinaendelea kuzuia vyombo vya habari vya kimataifa kufanya kazi na kuripoti ndani ya Gaza.
“Upatikanaji wa waandishi wa habari wa kimataifa kuripoti kwa uhuru kutoka Gaza lazima utolewe,” wakala huo alisema.
Sambamba na hilo, Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, alisema inasikitishwa sana na kitendo cha Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) kusimamisha shughuli za mtandao wa habari wa Al Jazeera katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Idhaa hiyo yenye makao yake makuu nchini Qatar ilishutumiwa kwa kutangaza “vitu vya uchochezi” ambavyo “vilikuwa vinadanganya na kuchochea ugomvi”, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa ambazo zilinukuu shirika rasmi la habari la Palestina Wafa.
Maendeleo hayo yanakuja huku kukiwa na “mwenendo wa kutatanisha” wa kukandamiza uhuru wa maoni na kujieleza katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, OHCHR ilisema, na kuitaka PA “kubadili mwelekeo na kuheshimu wajibu wake wa sheria za kimataifa.”