Waendesha baiskeli Geita watembezwa kuangalia mradi wa bilioni 4.450

Serikali Mkoani Geita imeendelea kuwa kivutio kwa wakazi wa Mkoa humo hii ni Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuleta kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 4 kujenga shule ya wasichana ili kuondokana na changamoto mbalimbali za kielimu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Geita , Hashim Komba wakati alipofanya ziara ya kuwatembeza waendesha Daladala (Baiskeli) katika Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ukiwemo mradi wa shule ya Sekondari ya wasichana Geita Girls pamoja na ukarabati wa Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita ambapo kiasi cha shilingi milioni 900 kimetumika kukarabati hospitali hiyo.

” Leo tuliona nyinyi kama vijana mate nafasi ya kuona kwenye sekta ya elimu jambo ambalo limefanyika hapa tumeambiwa na Afisa Elimu wetu wa sekondari ya kwamba ni Bilioni 4 na Milioni 100 zimeshawekwezwa kwenye eneo hili , ko nyie mkirudi huko kazi yenu kubwa ni kwenda kuwaambia wananchi wenzetu wa wilaya ya Geita , ” DC.Komba.

Kwa upande wake Rashid Mhaya ambaye ni Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Manispaa ya Geita amesema shule hiyo itaghalimu jumla zaidi ya shilingi Bilioni 4 fedha ambazo zimeletwa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza walipokea bilioni tatu ambazo zilijenga Madarasa 10 pamoja na Matundu 16 ya vyoo .

“Jumla ya shilingi Bilioni 4 milioni 400 na 50 fedha ambazo zimeletwa katika awamu ya Pili awamu ya kwanza tulipokea bilioni 3 ambazo tulijenga madarasa 10 tutayaona yako upande huo na chini yake kidogo kuna matundu 16 ya choo kwa ajili ya vijana wetu lakini katika awamu hiyo hiyo tulijenga Maabala nne kwa sababu shule yetu ni shule ya mchepuo wa sayansi , ” Afisa Elimu Sekondari Halmashauri Manispaa ya Geita, Mhaya.

Baadhi ya Viongozi wa Daladala (Baiskeli) wameipongeza serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada alizozieweka katika sekta mbalimbali ndani ya wilaya ya Geita ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.

Related Posts