Mwandishi Wetu.
WANANCHI wa kijiji cha Ikuvilo kata ya Luhota wilaya ya Iringa vijijini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Hayo yamesemwa na mdau wa maendeleo na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wakili Sosten Mbedule mara baada ya kuhakiki taarifa zake.
Amesema, ni vema kila mwananchi kuhakiki taarifa zake ili aweze kutumia haki zake za msingi kuchagua viongozi wanaowataka
“Wananchi wa kijiji cha Ikuvilo wanatakiwa kutumia fursa hii, kwenda kwenye kituo cha kupiga kura na kuhakiki taarifa zake, kuepuka usumbufu hapo badae,” amesema na kuongeza
“Wale ambao kadi zao zimeharibika au kupotea ofisa uchaguzi atawasaidia taratibu za kufanya ili wapate kadi mpya,” amesema Wakili Mbedule
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba 2025, wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.