*Prof Sedoyeka aweka mikakati ya kuibua vipaji vya wanafunzi
Na Chalila Kibuda
Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimeweka mikakati ya kuendeleza michezo nchini kwa kuwa uwanja wa kisasa katika Kampas ya Babati.
Hayo aliyasema Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka wakati akizungumza waandishi wa Habari katika Kampas Mpya ya Chuo hicho Babati mkoani Manyara.
Amesma malengo ya uwanja huo kuweza kutumika katika michuano ya mwaka 2027 ambapo Tanzania ni mwenyeji katika masndano ya Afcon.
Profesa Sedoyeka amesema licha ya kuwa na uwanja wa watakuwa na nyumba kwa ajili ya wanamichezo Hostel hivyo wakiwa hapo hawatalazimika kuchukua hoteli.
Hata hivyo amesema kuwa licha ya kuwa na kiwanja cha mpira wa miguu pia watakuwa na viwanja vya michezo mingine kwa ajili ya kila mtu kunyesha kipaji chake wakiwemo wanafunzi wa IAA.
Profesa Sedoyeka amesema kuwa viwanja hivyo vitatumika kwa ajili ya kulea vipaji vya watoto katika kipindi shule zimefunga watatumia kufanya mazoezi.
Amesema kuwa malengo ya Chuo kuwa na vitu vya kushikika vya kufanya vijana kutengeneza vipaji vya michezo na huku wakiwa na taakuma zingine za kuwasaidia katika kuendesha maisha yao.
“Natamani kuona viwanja vyetu hivi tunapata wachezaji wa ambao watatangaza Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Taifa kwa ujumla”amesema.Profesa Sedoyeka