MBEYA; WAFANYAKAZI WAWILI WA TANESCO WASHIKILIWA NA POLISI

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na maafisa wa shirika la umeme nchini [tanesco] linawashikilia watuhumiwa wawili Movin Joseph Mwaholi [53] Mfanyabiashara wa vifaa vya umeme na Rehema Jamson Silia [42] Mfanyabiashara wa chuma chakavu, mkazi wa nzovwe kwa tuhuma za kukutwa na miundombinu ya umeme na maji.
Watuhumiwa walikamatwa Januari 02, 2025 katika oparesheni ya pamoja iliyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na maafisa wa shirika la umeme [TANESCO] kanda ya nyanda za juu kusini katika eneo la uwanja wa ndege wa zamani mtaa wa Block T Jijini Mbeya katika godown la mfanyabiashara Movin Joseph Mwaholi.
watuhumiwa walikutwa na vifaa mbalimbali vya umeme na maji ikiwemo harking hons 57pcs, spindle 128 pcs, inlate cape 35 pcs, gaskate cover, bolt, nuts, copper wire, aluminium wires, bib tape ¾ 43 pcs, gate valve ¾ 35 pcs, black nut ¾ 5 pcs, mfuniko wa mita 1 pc. Baadhi ya vifaa hivyo ni vile vilivyofunguliwa kwenye miundombinu ya umeme, Transformer na miundombinu ya maji ambayo imetambuliwa na maafisa wa TANESCO na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kutoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye tabia ya kuhujumu miundombinu ya nchi ikiwemo ya Umeme na Maji kuacha mara moja kwani uhalifu hauna nafasi wala haulipi ni vyema wakafanya shughuli nyingine halali. Vitendo hivyo wanavyofanya vinarudisha nyuma juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo Jeshi la Polisi litaendelea na oparesheni hii na wale wote watakaobainika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria ikiwepo kufikishwa mahakamani.

Imetolewa na:

Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.

Related Posts