BALOZI KOMBO AONGOZA MKUTANO WA MAWAZIRI WA ASASI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA SADC

Mkutano wa Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umefanyika Zanzibar tarehe 04 Januari, 2025 chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thatib Kombo akishirikiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Zambia na Malawi ambao ni wajumbe wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ Troika).

Mkutano huo ni maalum kwa ajili ya Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo utakaofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 05 Januari, 2024.

Mkutano huo ulitoa mapendekezo ya namna SADC inavyoweza kuisaidia Jamhuri ya Msumbiji kukabiliana na changamoto za kisiasa zinazoendelea nchini humo, ambapo mapendekezo hayo yanatarajiwa kupitishwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Organ Troika utakaongozwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Msumbiji imekumbwa na machafuko ya kisiasa kufuatia chama cha upinzani kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 09 Oktoba, 2024.













Related Posts