Na Issa Mwdangala
Kamanda Senga aliwasisitiza askari hao kufanya kazi kwa kuzingatia Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu na kutenda kwa kuzingatia sheria za nchi bila kumuonea mtu na kutokuwa na muhali kwa wahalifu.
Naye, Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban aliwataka askari hao kuwapa elimu wananchi wanaofungua kesi kufika mahakamani kwa lengo la kutoa ushahidi ili kuweza kupata mafanikio ya kesi hizo na iwe fundisho kwa jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Songwe (ACP) Nicholas Livingstone aliwasisitiza Askari hao kufanya doria na misako yenye tija ili ilete mafanikio ikiwa ni pamoja na kuendelea kujenga umoja na ushirikiano kwa wananchi kwa lengo la kupata taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.