Kinda Mbongo anakiwasha tu Australia

BEKI wa kulia Mtanzania, Kealey Adamson anayekipiga katika timu ya Macarthur ya Australia amekuwa mhimili mkubwa wa timu hiyo kwenye eneo la ulinzi.

Kinda huyo mwenye miaka 20 ni Mtanzania mwenye asili ya Australia na aliwahi kucheza klabu moja na Charles M’mombwa ambaye amekuwa akiitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Timu hiyo iko nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi baada ya mechi 11 ikishinda tano, sare tatu na kupoteza tatu na imeruhusu mabao 15.

Mechi 10 za mwisho ilizocheza timu hiyo ametumika kwa dakika 887 na amekuwa akianza na kuonyesha kiwango bora akiendelea kuaminiwa kwenye kikosi hicho chini ya kocha Mile Sterjovski ambaye ni raia wa Australia.

Baada ya mchezo wa juzi Januari 01, Macarthur kuondoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya WS Wanderers kinda huyo alionyesha kiwango bora na kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo akipongezwa na timu yake.

“Ilikuwa vita ya kishujaa kutoka kwa beki wetu wa kulia, ambaye amejishindia tuzo ya mchezaji bora wa mechi kutoka kwa wanachama, hongera sana, Kealey.” uliandikwa ujumbe huo ukiambatana na picha yake

Ligi ya nchi hiyo waliomaliza msimu katika nafasi za juu, wanacheza mchujo wa kuwania ubingwa.

Related Posts