MBUNGE KILANGO ASEMA WANANCHI WA JIMBO LA SAME MASHARIKI WANATOA MACHOZI YA FURAHA

SAME.

MBUNGE wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela amesema wananchi wa Same wanatoa machozi ya furaha, kutoka na Barabra ya Same- Mkomazi kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami kwani shida kubwa inayowakabili ni barabara hivyo ujenzi wake ni ukombozi mkubwa kwa maisha yao.

” Leo mama Samia Suluhu Hassan anaandika historia ya kuikomboa Wilaya ya Same kwa kujenga barabara ya lami na ujenzi wake ukikamilika  utaongeza  uzalishaji wa mazao ya tangawizi, ndizi, matunda na mpunga”, amesema Kilango.

” Waziri Ulega asilimia 72 ya tangawizi inayozalishwa Tanzania inatoka Same hivyo barabara hii itarahisisha usafiri na usafishaji na kuwawezesha wananchi kuyafikia masoko kwa urahisi”, amesisitiza Kilango.

Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta amesema barabara ya Ndungu-Mkomazi Km 36 ni sehemu ya barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa Km 100.5  ambayo ni barabara ya kimkakati inayounganisha mkoa wa Tanga na Kilimanjaro ambapo km 96.5 ziko mkoa wa Kilimanjaro na Km 4 ziko mkoa wa Tanga hivyo kukamilika kwake kutachochea  shughuli za kilimo, uvuvi, biashara na utalii  katika hifadhi ya mkomazi na milima ya Pare.

 

Related Posts