Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa COREFA Robert Munisi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalumu ambao umefanyika makao makuu ya ofisi za chama hicho kilichopo eneo la kwa Mathias Wilaya ya Kibaha na kuhudhuliwa na viongozi mbali wakiwemo viongozi wa soka la wanawake kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali ya maendeleo ya mchezo huo.
Mwenyekiti huyo amesema kwamba lengo kubwa la kukutana katika mkutano huo ni kwa ajili ya kuweka mikakati na mipango madhubuti katika ya uongozi wa COREFA pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani ili kuweza kuona namna nzuri ya kuripoti habari za mchezo wa soka, kusikiliza maoni, changamoto, pamoja na kuelezea mafanikio ambayo yamepatikana kwa Corefa.
Munisi amebaainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuweza kushirikiana na waandishi wote wa Mkoa wa Pwani katika kuhakikisha wanatangaza na kuhabarisha jamii mambo mbali mbali ambayo ynafanywa na chama ikiwemo kuweka mipango ya kuripoti habari za mchezo wa soka la vijana, wanawake, na soka la ufukweni ikiwa sambamba na kushirikiana katika mambo mbali mbali ambayo yataweza kuletaa tija katika nyanja ya mchezo wa soka ndani ya Mkoa wa Pwani.
“Kimsingi mimi kama Mwenyekiti nimefarijika sana kukutana naa ndugu zangu waandishi w habari ambapo lengo kubwa ni kuzungumza mambo mbali mbali ikiwemo mafanikio ambayo tumeweza kuyapata tangu niweze kuingia madarakani na kitu kikubwa tumeweza kufanya mambo mengi ikiwemo kupata ofisi yetu eneo la kwa mathiasi japo kwa sasa tumepanga lakini dhumuni etu kubwa ni kujenga ofisi yetu ya Corefa ambaayo itakuwa ni ya kudumu,”alisema Mwenyekiti Munisi.
Aidha alisema kwamba kwa sasa lengo lao kubwa ni kuwa ni uwanja mkubwa wa kisasa wa mpira wa miguu ambao utatarajiwa kujengwa katika kata ya viziwaziwa Wilaya ya Kibaha na kwamba tayari wameshapokea barua ya kupewa eneo kutoka kwa uongozi wa Halmashauri ya mji Kibaha kwa ajili ya kuweza kunegaa uwanja huo ambao kwa upande wao utakuwa ni moja katika ya vitega uchumi vya chama chao.
Kadhalika amesem kwamba sasa wameshaanza kutekeleza maagizo ambayo yametolewa ba shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) ya kuanzisha ligi ya soka la ufukweni, ikiwa sambamba na kukuza soka la vijana pamoja na soka la wanawake amablo kwa sasa katika Mkoa wa Pwani linafanya vizuri ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alitumia mkutano huo kudhamini kwa dhati juhudi za mwandishi wa habari za michezo Mkoa wa Pwani Abdalalah Zalala kwa kumpogeza na kumkabidhi cheti na kiasi cha shilingi laki moja ikiwa kama ni moja ya motisha katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuandika na kuripoti habari za mchezo wa soka kwa kujitolea na weledi.
“COREFA inatambua mchango wa Mwandishi wa Habari za michezo Abdallah Zalala na leo tunamkabidhi zawadi ya fedha lakini tutaendelea kuwashika mkono Waandishi wote ambao watakuwa wanaandika zaidi habari za michezo za Mkoa wa Pwani,”amesema Munisi
Pia Munisi amebainisha kwamba Chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) kimejipanga na kujizatiti zaidi katika kuhakikisha mpira unachezwa katika Wilaya zote kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanunu, miongozo na katiba ya vyama ngazi ya Wilaya, Mkoa, pamoja na Taifa ili kuepusha migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza na kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega na wadau wa mchezo wa soka ndani ya Mkoa wa Pwani lengo ikiwa mashindano na ligi zote zifanyike kama ilivyopangwa kwa mujibu wa ratiba ya TFF.