TIMU ya soka ya wanawake ya vijana U17 ya JKT Queens inatarajiwa kuzindua michuano ya CAF kanda ya Cecafa inayoanza kesho kwa kuvaana na City Lights FA ya Sudan Kusini kwenye mchezo wa Kundi A wa michuano hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi Dar es Salaam.
JKT Queens imepangwa kundi moja sambamba na Wasudani Kusini hao na Bahir Dar Kenema FC ya Ethiopia na Kenya Academy of Sports ya Kenya, wakati Kundi B lina timu za TDS Girls Academy ya Tanzania, Aigle Noir FC ya Burundi, Boni Consilli Girls Vocational Team ya Uganda na Hilaad FC ya Somalia.
Michuano hiyo iliyopewa jina la ufupisho la GIFT ( U-17 Girls Integrated Football Tournament) ni mipya ikifanyika kwa mara ya kwanza nchini ikishirikisha timu nane za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na CAF, mashindano hayo ni sehemu ya mkakati shirikisho hilo la soka Afrika kukuza usawa wa kijinsia na kuwezesha kizazi kijacho cha wechezaji wa kike.
CAF imedhamiria kuongeza ushiriki wa wasichana katika soka Afrika.