Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua Skuli ya Sekondari ya Makoba Kaskazini Unguja

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 06, 2025 amefungua Skuli ya Sekondari ya Makoba iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Ujenzi wa Shule hiyo ambao umefikia asilimia 100 umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.1 ambazo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi.

Related Posts