Waziri Mkuu wa Canada kujiuzulu?

JUSTIN Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada, huenda akatangaza kujiuzulu ndani ya siku chache, kulingana na ripoti za vyombo vya habari. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Anafikiria kujiuzulu kama kiongozi wa chama tawala cha Liberal, na kumaliza miaka yake tisa kama waziri mkuu.

Ni kufuatia miezi kadhaa ya shinikizo kutoka kwa wabunge wa chama chake.

Mwezi uliopita, waziri wake wa fedha alijiuzulu, akitoa sababu za kutokuelewana kuhusu jinsi ya kukabiliana na tishio la Donald Trump la kutoza ushuru mkubwa kwa bidhaa za Canada.

Kura za maoni zinaonyesha chama cha Liberal cha Trudeau kipo nyuma ya chama cha Conservatives huku uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Zaidi ya dazeni ya wabunge wake wamemtaka aondoke madarakani, huku kura za maoni zikionyesha thuluthi mbili ya wapiga kura wanampinga.

Gazeti la Globe and Mail linaripoti kwamba anaweza kutangaza nia yake ya kujiuzulu kabla ya kikao cha chama chake siku ya Jumatano, ili kuepusha dhana kwamba wabunge wake walimlazimisha kuondoka.

Vyanzo vyao vinasema, haijulikani ikiwa Trudeau ataondoka moja kwa moja au ataendelea kuwa Waziri Mkuu hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.

Lakini vyanzo hivyo vimesisitiza kuwa bado hajafanya uamuzi wa mwisho juu ya mustakabali wake.

Aliingia madarakani mwaka 2015, akiwa na umri wa miaka 43 wakati huo, aliahidi aina mpya ya siasa inayozingatia sera za wazi juu ya uhamiaji, kuongeza kodi kwa matajiri na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

About The Author

Related Posts