Asia Mustapha ni binti ambaye ameishi kwa takribani miaka 20 bila figo zote mbili, akitegemea huduma ya kusafisha damu kwa njia ya mashine (dialysis).
Mwanzoni, huduma hiyo ilikuwa ya gharama kubwa, lakini serikali kupitia Wizara ya Afya iligharamia matibabu hayo kwa miezi minne.
Hata hivyo, baada ya kipindi hicho, hakukuwa na msaada zaidi wa moja kwa moja.
Kwa sasa, Asia hawezi kutembea kutokana na mifupa yake kutoboka, hali inayosababishwa na ugonjwa wake wa muda mrefu.
Aidha, Asia alipoteza wazazi wake wote wawili, ambao walikuwa tegemeo lake kubwa maishani.
Asia ameomba nafasi ya kuonana na Rais Samia ili kueleza changamoto zake kwa kina, akihitaji msaada wa hali na mali kwa ajili ya chakula, pampers na nauli ya kusafiri mara tatu kwa wiki kwa ajili ya dialysis.
Kwa yeyote aliyeguswa, unaweza kumsaidia Asia kupitia namba ya simu 0656684431 (Asia Sali).