Mlimba kutoa mikopo ya asilimia 10 ya Bil.2.2

Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro imetenga zaidi ya shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya mikopo ya asilimia Kumi ya vijana,wanawake na walemavu .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya halmashauri ya Mlimba Jamari Idrisa amesema mikopo hiyo inatarajiwa kuinua uchumi wa wananchi wa eneo hilo .

Amesema kwa awamu ya kwanza wametoa mikopo yenye Thamani ya Milioni mia Saba kwa vikundi 49 ambayo vimekidhi vigezo.

Jamari amesema kabla ya mwaka wa fedha 2024/2025 kumalizika mwezi June mwaka huu fedha zote zitakuwa zimetolewa kwenye vikundi ambapo anatoa wito Kwa wananchi kuendelea kuuunda vikundi Ili kuwa na sifa ya kupata mikopo inayotolewa na halmashauri hiyo.

Mkuu Wilaya ya Kilombero Dunstan Kyobya anatoa tahadhari ya ureshwa wa mikopo hiyo Ili watu wengine waweze kunufaika.

Amesema awali mikopo hiyo ilisitishwa Kwa sababu ya Watu kushindwa kurejesha kwa wakati hivyo ili Watu wengine waweze kukopa ni lazima fedha zirudishwe

Naye Kamanda wa Takukuru Wilaya Kilombero Eufrasia Kayombo amesema Serikali haitasita kumchukulia hatua za kisheria Mtu yeyote atakaye kaidi zoezi la urejeshaji wa mikopo hiyo kwa wakati.

Amesema ni lazima katika vikundi kuendelea kuhamasisha hasa matumizi sahihi ya Pesa zitumike kama zilivyotarajiwa Ili Lengo la Serikali la kuwainua kiuchumi wananchi litimie

Juma Mpole mnufaika wa mikopo hiyo anaishukuru Serikali ya awamu ya sita na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha mikopo hiyo.

Amesema awali hakuwa na mtaji wala kaz maalum ya kumuingizia kipato lakini Kwa Sasa amepata pikipiki ambayo tamuingizia pesa.

Related Posts