Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema iwapo kuna kiongozi, mwanachama au mgombea anatuhumiwa kukiuka miongozo ya uchaguzi, taarifa ya malalamiko yawasilishwe rasmi kwa mamlaka ili kudhibiti changamoto hiyo.
Mnyika amesema hayo leo Jumanne, Januari 7, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Amewaomba wafuasi, wagombea na wanaowaunga mkono kufuata na kuzingatia miongozo hiyo ili kuwa na uchaguzi huru na wa amani.
Mnyika amesema jumla ya wagombea 300 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali ngazi ya Taifa ikiwamo uenyekiti, makamu uenyekiti Taifa, mabaraza na kamati kuu.
“Mchakato wa kuwasaili na kufanya uteuzi unafanywa na kamati kuu,” amesema Mnyika. Usaili kwa mabaraza utaanza Januari 10.
Endelea kufuatilia Mwananchi.