Tetemeko La Ardhi Laua 53 Magharibi mwa China – Global Publishers



Tetemeko kubwa la ardhi limeua watu 53 leo Jumanne Januari,  7 2025 huko Tibet, China na kuwaacha wengine wengi wakiwa wamekwama chini ya vifusi. Tetemeko hili limefuatiwa na mitetemeko midogo kadhaa ambayo imetikisa maeneo ya magharibi mwa China na nchi jirani ya Nepal.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Xinhua, watu 62 waliripotiwa kujeruhiwa, taarifa iliyotolewa na makao makuu ya misaada ya maafa ya kikanda imesema.


Wizara ya Usimamizi wa Dharura ilisema kuwa zaidi ya wafanyakazi wa uokoaji 1,500 wa zimamoto na uokoaji walisambazwa kutafuta manusura waliokwama kwenye vifusi.
Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani (USGS) lilisema kuwa tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 7.1 na lilikuwa na kina kifupi cha kilomita 10 (maili 6). Hata hivyo, China ilikadiria ukubwa wake kuwa 6.8.











Related Posts