WANAWAKE WATAWALA PROMOSHENI YA SANTA MIZAWADI KUTOKA AIRTEL

Meneja Mauzo kwa wafanyabiasha wadogo wakati na wakubwa wa Airtel Money, Janeth Kwilasa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na wakati wa promosheni ya Santa Mizawadi iliyechezeshwa leo Januari 07, 2025 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Ubunifu kutoka Airtel, Husein Simba. Na Kulia ni Muwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Elibariki Sengsenga.

Meneja Mauzo kwa wafanyabiasha wadogo wakati na wakubwa wa Airtel Money, Janeth Kwilasa akizungumza na mteja wakati wa promosheni ya Santa Mizawadi iliyechezeshwa leo Januari 07, 2025 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Ubunifu kutoka Airtel, Husein Simba.

Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Airtel imebadili imewapa furaha wanawake kwa bahati zao za kutumia mtandao wa Airtel katika droo ya tatu ya santa mizawadi ambapo katika droo hiyo iliyochezeshwa leo Jumanne Mwanaume mmoja ndio ameibuka mshindi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 07, 2024, Meneja Mauzo kwa wafanyabiasha wadogo, wakati na wakubwa wa Airtel Money, Janeth Kwilasa amesema kuwa Washindi wa Promosheni ya leo wanabahati kubwa kwani ni promosheni ya kwanza tangu mwaka uanze.

Mshindi wa pikipiki Emanuela Vulwa kutoka jijini Arusha amefanikiwa kuandika historia kwa kutwaa pikipiki hiyo katika wiki ya tatu tangu promosheni ya Santa ichezeshwe.

Katika droo ya tatu ya Santa Mizawadi kutoka Airtel ambayo imechezeshwa na Janeth Kwilasa, amemtangaza Angelina Bahati mwenye bahati yake kutoka Arusha kuwa mshindi wa Luninga inchi 55 (Smart Tv).

Na Mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni Moja Kutoka Airtel Santa Mizawadi ni Elizabeth Robart kutoka Mkoani Singida na washindi wawili wa Simu Janja ni Subira Omari kutoka Tanga na Habibu Abdi kutoka Mkoa wa Kagera.

Janeth amesema kuwa Droo hiyo itaendelea kufanyika kwa wiki nyingine ya mwisho kwa lengo la kuwapa wateja wao zawadi mbalimbali ikiwemo fedha, pikipiki, runinga, smartphone kwa wale ambao wanatumia huduma za Airtel kwa njia tofauti tofauti.

Amesema washindi watajishindia zawadi kwa kufanya miamala kila siku kwa kipindi cha Sikukuu ya Kristmasi na Mwaka mpya kwa kutuma na kupokea pesa, kulipia bili mbalimbali na kununua muda wa maongezi pamoja na kujiunga na vifurushi.

Ameongeza kuwa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi inalenga kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia Airtel katika msimu wote huu wa Sikukuu.

Ameelezea jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Janeth amesema Kwa Wakala wa Airtel anatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha na Kwa mteja anachotakiwa kufanya kununua bando, kulipa bili, kutuma na kutoa fedha, kununua muda wa maongezia au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60# au kupitia ‘My Airtel App’.

Ameongeza kuwa washindi wote watafikishiwa zawadi popote walipo baada kuoigiwa simu na huduma kwa wateja yaani namba 100 na baada ya taratibu kukamilika.

Related Posts