Wakati Serikali iliendelea na maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa Madiwani,wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu 2025 vijana wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kushiriki masuala muhimu ya nchi ili kuleta maendeleo.
Wito huo umetolewa na Godlisten Mramba ambaye ni mwimbaji nyimbo za injili wakati akizungumza na wahadishi wa habari Mjini Morogoro ambapo amesema vijana wengi hawajitokezi katika masuala ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, uchaguzi kutokana na wengi wao kuona masuala hayo ni ya wazee tuu jambo ambalo halina linarudisha nyuma kundi hilo kusukuma gurudumu la maendendeleo.
Mramba amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo wameandaa kongamano la kidini la Vyuo na Vyuo Vikuu litakalo fanyika February 7 mwaka huu 2025 eneo la bigwa Mkoani Morogoro.
Schola Pius meneja wa kongamano hilo amesema wanatarijia kuwafikia vijana zaidi ya elfu kumi ambapo watapata fursa ya kutoa hamsa masuala ya afya,uchumi ,elimu na Kushiriki katika uchaguzi.
Vijana wengi wamekuwa na mtazamo mmoja tu wa kusubiri Ajira Serikalini hali ambayo inasababisha Vijana wengi kuwa tegemezi bali Vijana wakipewa maarifa wanaweza kujisimamia katika kuendeleza maendeleo hata pasipo Ajira Serikalini
Kwa Upande wake Mchungaji wa kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) Chritina Kila amesema viongozi wa dini pia wanawajib kushirikiana na WAZAZI na walezi katika kuhakikisha vijana wanakuwa katika maadili mazuri.
Aidha amesema kuwa Vijana wengi wamekuwa na wimbi la mmonyoko wa Maadili Hali ambayo inaweza kuchangia ukatili kwa Baadhi ya watu na kama kanisa watasimama vyema kuhakikisha wanatoa elimu ya Maadili na ukatili wa kijinsia