Dar es Salaam. Mwanaume asiyeamini kuwa Mungu yupo kutoka nchini Nigeria, Mubarak Bala (40) ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani kwa tuhuma za kumtukana Mungu kupitia Facebook mwaka 2020.
Mubarak alikamatwa Aprili 28, 2020, kwa tuhuma za kukufuru dini na uchochezi kutokana na machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii.
Aprili 2022, alihukumiwa kifungo cha miaka 24 gerezani baada ya kukiri makosa 18, ikiwa ni pamoja na kukufuru na uchochezi.
Hata hivyo jana Januari 7, 2025, aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani. Baada ya kuachiliwa amesema usalama wake bado uko hatarini kutokana na vitisho.
“Wasiwasi kuhusu usalama wangu upo kila wakati,” aliambia BBC katika mahojiano yake.
Mwanaume huyo kwa sasa anaishi katika nyumba ya hifadhi, huku mawakili wake wakidai maisha yake yako hatarini ikiwa atarejea kuishi katika jamii.
Endelea kufuatilia Mwananchi.