Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(kulia), akiagana na Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe.Yasushi Misawa, baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania na Japan zitaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kijamii kwa faida ya nchi hizo mbili huku Mhe. Balozi Misawa kwa upande wake, akisema Tanzazania na Japani zina uhusiano wa kihistoria ambao nchi yake itauendeleza kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi yake.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Dodoma)