Mambo matatu yanayomsubiri Rais mpya Ghana

Dar es Salaam. John Mahama ameapishwa jana Jumanne, Januari 7, 2025 kuwa Rais wa awamu ya tatu, huku taifa hilo lilikabiliwa na changamoto ya uchumi.

Rais Muhama katika kampeni zake alijinadi kukabiliana na anguko la kiuchumi, rushwa na ukosefu wa ajira nchini humo.

Kiongozi huyo mwenye miaka 65, amewahi kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha Julai 2012 na Januari 2017 akipokea kijiti kutoka kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Nana Akufo Addo.

Mahama amekuwa Rais wa kwanza kuapishwa katika nafasi hiyo tangu Rais John Evans Atta alipofariki mwaka 2012 ambapo aliingia madarakani kwa kipindi cha muhula mmoja na baadaye alishinda uchaguzi mwaka 2012.

Rais Mahama ameingia madaraka akiwa na matumaini ya kuleta mabadiliko katika nchi hiyo, huku kipaumbele cha wananchi ni kutaka uchumi bora na ajira kwa raia wa Ghana.

Ofisa mwandamizi wa utafiti katika masuala ya habari, Inncocent Appiah amesema anatarajia Rais Mahama ataongoza kwa kufuata vipaumbele vyake kwa uwazi na weledi katika kuinua uchumi wa viwanda.

“Ninaimani katika sera ambazo zinaleta matumaini, kukuza uchumi wa ndani na kuijumuisha jamii, ni mambo ambayo yatasaidia kuongeza mapato na kuletea maendeleo ya raia wa Ghana.

Viongozi mbalimbali wa nchi walihudhuria sherehe hizo za uapisho akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Philip Mpango.

Related Posts