MSHAMBULIAJI wa Yanga Sc Clement Mzize, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa wiki wa michuano ya Klabu bingwa Afrika na Shirikisho la Soka Afrika (CAF)
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa akivutia klabu nyingi kubwa kutoka nje na ndani ya Afrika kwa muda mrefu na ameendelea kujijengea sifa kwa bora anaozidi kuuonyesha katika miezi ya hivi karibuni.
Mabao mawili dhidi ya TP Mazembe yamefanya idadi ya mabao matano katika Ligi ya Mabingwa msimu huu yakiwa matatu ya raundi mbiliĀ za awali, yakiweka hai tumaini la Yanga kufuzu hatua ya robo fainali.
Goli lake la kwanza lilikuwa shuti la mbali la kuvutia kutoka mita 30, lililoelekea moja kwa moja kwenye kona ya juu ya wavu ambalo lilisawazishia Yanga kabla ya kufunga goli la pili na kutoa pasi ya mwisho iliyozaa goli moja huku Aziz Ki akiifungia Yanga goli moja na kuweka idadi ya goli 3 – 1 katika mechi ya nne ya hatua ya makundi iliyopigwa wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.