Mkuu wa shule awafungia geti wanafunzi wasiolipa ada, Polisi waingilia kati

Uamuzi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St Annes’s Girls nchini Kenya kuwafungia wanafunzi walioripoti shuleni bila kulipa ada umechukua sura mpya baada ya wananchi kuhoji utaratibu huo huku wanaharakati na polisi wakiingilia kati.

Mkuu huyo wa shule, Veronika Muli jana Jumanne Januari 8, 2025 aliwazuia wanafunzi wa kike ambao walikuwa wamewasili shuleni hapo wakitoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Wanafunzi hao walilazimika kubaki nje ya geti hadi sa tatu usiku.

Mmoja wa wazazi aliyezungumza na gazeti la Nation, amesema wanafunzi hao waliwasili shuleni hapo mapema mchana kabla ya muda ulioweka wa kuripoti saa 10:00 jioni, lakini kutokana na sintofahamu hiyo walizuiwa kuingia.

“Hii siyo mara ya kwanza inatokea. Nilikuwa hapa mapema na nilirudi kwa sababu mkuu wa shule alitangaza hawezi kuzungumza nami  kwani nilikuja kwa ajili ya kuwahamisha watoto wangu wawili kwenda shule nyingine.

Mtetezi wa Haki za Binadamu, Dennis Esikuri alisema alikaa na wanafunzi hao nje ya geti huku akiwaomba walinzi kuwafungulia geti lakini licha ya juhudi hizo, ziligonga mwamba mpaka saa tatu usiku  polisi walipofika eneo hilo.

Hivi karibuni Rais wan chi hiyo, William Ruto na Katibu Mkuuu, Julius Migos waliagiza hakuna mwanafunzi yoyote kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kutokamilisha ada.

Related Posts